Monday, July 29, 2013

WAANDISHI WA HABARI WATEMBELEA KAMPUNI YA BIA (TBL) MBEYA


Waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya wakitembelea kapuni ya Bia TBL
Moja ya watumishi wa kampuni hiyo ya Bia akiwaeleza waandishi wa habari jinsi bia inavyotengenezwa
Ziara inaendelea

 Meneja kiwanda cha kampuni ya Bia TBL  Mbeya Nicolaus  Kanyamala akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea kiwanda hicho
Baadhi ya wa watumishi wa kampuni ya Bia wakijitambulisha mbele ya waandishi wa habari

Meneja uhusiano wa TBL Dorris Malulu akizungumza na waandishi wa habari
Meneja masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) Kanda ya Mbeya, Raymond  Degera, akielezea mafanikio ya kampuni ya Bia

Mpishi Mkuu wa Bia wa Kampuni ya Tbl, Tito alisema Sheria za Tanzania zinatakiwa kusimamiwa ipasavyo kuhusu matumizi ya Vilevi kwa kuwashtaki wanaozidisha pombe na wengine wanaokunywa mida ya kazi na kuleta usumbufu kwa wengine.

Wanahabari walipata fursa ya kuelezwa sheria za unywaji wa Pombe na madhara yake, umri wa mtu kuanza kunywa pombe pamoja na madhara yake ambapo baada ya zoezi hilo walitembelea maeneo mbali mbali ya Kiwanda hicho.
Baada ya kutembelea kiwanda  sasa ilifika wakati wa kuonja Bia na kuitambua radha yake
Unaonja na kutaja ni bia gani kama ni NDOVU au KILIMANJARO kunaalama za rangi zimewekwa katika grass
Mwandishi wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango akionja na kujaza katika fomu kuwa hiyo aliyoinja ni Bia gani
 Meneja kiwanda cha kampuni ya Bia TBL  Mbeya Nicolaus  Kanyamala akimkabidhi zawadi Joseph mwaisango mara baada ya kuibuka mshindi wa uwonjaji bia
 Meneja kiwanda cha kampuni ya Bia TBL  Mbeya Nicolaus  Kanyamala akimkabidhi zawadi Emmanuel Madafa baada ya kushinda uonjaji wa Bia
Mshindi wa pili Joachim Nyambo akipokea zawadi yake toka kwa meneja wa kampuni ya bia 
Picha ya pamoja


ZAIDI ya Tani 60,000 za Shayiri  zinatarajiwa kuvunwa kutoka kwa Wakulima wa  Kanda ya Nyanda za Juu Kusini baada ya kupatiwa mafunzo juu ya kilimo cha mazao yenye tija na uwepo wa soko la uhakika.
Aidha zaidi ya Wakulima 400 kutoka Kanda hiyo ndiyo walionufaika na Kilimo hicho na kujihakikishia Soko la zao ambalo hutumika zaidi katika utengenezaji wa Vinywaji moto ambavyo ni Bia na uzalishaji mwingine kutokana na uwepo wa Viwanda vikubwa vya kuzalisha vinywaji hivyo.
Hayo yalibainishwa juzi na Meneja masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) Kanda ya Mbeya, Raymond  Degera,wakati wa Ziara ya Waandishi wa Habari katika Kiwanda cha Bia kilichopo Iyunga Jijini Mbeya.
Alisema  kutokana na uwepo wa Kiwanda cha Bia Mkoani Mbeya na kuhudumia Wananchi wa Kanda ya Nyanda za Juu kusini waliona si vema Malighafi zikatoka Nje ya Mikoa hiyo ili hali ardhi na hali ya Hewa inaruhusu kilimo cha mazao hayo na kuamua kutoa elimu namna ya kunufaika na Kilimo.
Degera alisema Kampuni  ilianzisha Programu ya kuwawezesha Wakulima kuhusu kilimo cha mazao yenye tija ambapo Wakulima wa Wilaya ya Mbozi, Sumbawanga na Iringa wanaofikia 400 ambao waliitikia na kuanza uzalishaji ambao baada ya mavuno kiwanda kitanunua moja kwa moja kutoka kwa wakulima ambao wanatarajia kuvuna Tani 60,000.
Kwa upande wake  Mpishi Mkuu wa Bia wa Kampuni ya Tbl, Tito alisema Sheria za Tanzania zinatakiwa kusimamiwa ipasavyo kuhusu matumizi ya Vilevi kwa kuwashtaki wanaozidisha pombe na wengine wanaokunywa mida ya kazi na kuleta usumbufu kwa wengine.
Alisema Utaratibu wa Nchi zingine  huwalazimisha wananchi wake kutumia Chupa mbili za Bia kwa siku na kwamba anayehitaji kuongeza zaidi ya hapo wauzaji huwakatalia, Sheria ambayo alishauri kutumika ili kuongeza uzalishaji na kuiondoa nchi katika majanga yanayotokana na ushawishi wa Pombe.
Aliongeza kuwa  kama wamiliki na watengenezaji wa Pombe wanahitaji wananchi wanywe kwa utaratibu ili waendelee kuwa wateja wao na  kusaidia kuchangia kodi kwa Taifa kutokana na Kampuni hiyo kuongoza kwa kuchangia kodi katika pato la Taifa.
Aidha katika Ziara hiyo Wanahabari walipata fursa ya kuelezwa sheria za unywaji wa Pombe na madhara yake, umri wa mtu kuanza kunywa pombe pamoja na madhara yake ambapo baada ya zoezi hilo walitembelea maeneo mbali mbali ya Kiwanda hicho.
Mbali na hilo wanahabari hao pia walishindanishwa kuonja Bia na kuzitambua kwa majina zoezi ambalo lilikuwa gumu kwa waandishi wengi huku Waandishi wanne wakiibuka washindi baada ya wawili kushika nafasi ya kuanza kwa kupata alama tatu kati ya Tano ambao ni Emmanuel Madafa na Joseph Mwaisango huku walioshika nafasi ya pili kwa kupata alama mbili kwa tano wakiwa ni Joachim Nyambo na Kenneth Ngelesi.

Chanzo:Mbeyayetu.blogspot.com


No comments:

Post a Comment