Monday, July 22, 2013

ARSENAL YAIBAMIZA NAGOYA GRAMPUS 3-1

ARSENAL YAIBAMIZA NAGOYA GRAMPUS 3-1

ase 9fdb4

The Gunners imefunga bao lake la 17 katika mechi tatu za kujiandaa na msimu nchini Japan jana, kutokana na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya timu ya zamani ya Arsene Wenger, Nagoya Grampus. (HM)
Olivier Giroud ameendeleza makali yake katika mwechi hizi za kujiandaa na msimu akitimiza mabao sita katika ziara ya Mashariki ya mbali, kabla mwanasoka wa kimataifa wa Japan, Ryo Miyaichi na Theo Walcott kufunga kitabu cha mabao.
Ilikuwa ni hatua nyingine nzuri ya kujiejengea kujiamini kwa The Gunners katika ziara yao ya majira ya joto, vaada ya ushindi wa 7-0 dhidi ya Indonesian Dream Team na 7-1 dhidi ya Vietnam XI.
Wenger, ambaye alijiunga na Gunners akitokea Nagoya Grampus mwaka 1996, alipata mapokezi mazuri kutoka kwa mashabiki wa Japan, ambao bado wanamkumbuka alipokuwa akifanya kazi na Nagoya, Dragan Stojkovic, mmoja wa wachezaji wake maarufu katika klabu hiyo.

Na kocha huyo wa The Gunners alishuhudia timu yake ikimpa raha mapema tu baada ya Giroud kufunga bao zuri la kichwa dakika ya tatu akimtungua kipa Seigo Narazaki kufuatia krosi ya Tomas Rosicky kutoka kulia.
Timu hiyo ya Ligi Kuu Englad ilitawala kipindi cha kwanza, Walcott, Ramsey na Miyaichi wote wakipoteza nafasi za kufunga kabla ya Gunners kufunga bao la pili dakika ya 26 baada ya Giroud kuchezewa faulo kwenye eneo la hatari.
Mikel Arteta alikwenda kupiga mkwaju wa penalti, lakini akakosa na mpira ukamkuta Miyaichi, aliyeukwamisha nyavuni na kuifanya Gunners iende kupumzika ikiwa inaongoza 2-0.


No comments:

Post a Comment