Wednesday, July 24, 2013

POLISI RUVUMA WAKAMATA MENO YA TEMBO WILAYANI TUNDURU


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjTz2VnGfi4xfdAW6IbQnDBsmZJqTk3YQSdgzVZOmSNJLnt6HH5V0DWvCT0_cE5Axhz1d4NKwxULMDZFlnbvVoBGcX711ymR5khzeUO9jOJAEYcJYZVW4vlS64AWSX8vKwfNjm5xXfdA3lK/s640/DSC00146.JPG

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki akiangalia pembe zilizokamatwa

JESHI la polisi mkoani Ruvuma kwa mara nyingine limefanikiwa kukamata nyara za serikali katika wilaya ya Tunduru tukio ambalo limetokea Julai 21 mwaka huu majira ya saa 11:40 alfajiri lililotanguliwa na tukio jingine lililotokea Juni 26 mwaka huu ambapo jumla ya meno 18 ya tembo yalikamatwa wilayani humo kwa ushirikiano wa jeshi la polisi na idara ya wanyamapori pamoja na wananchi wanaotoa taarifa za siri kwa vyombo hivyo vya ulinzi na usalama.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki amesema kuwa sik hiyo ya tukio askari polisi waliokuwa doria walifanya upekuzi kwenye mabasi yaliyokuwa yakianza safari alfajiri katika kituo kikuu cha mabasi cha mjini Tunduru ambapo katika basi moja lenye namba za usajili T315ABS aina ya Scania mali ya kampuni ya WAHIDA  walifanikiwa kukamata sanduku moja likiwa na nguo pamoja na vipande 21 vya meno ya tembo
Amesema kuwa vipande hivyo vya meno ya tembo vilikuwa na uzito wa kilogramu 34.45 na thamani yake ikiwa ni dola za kimarekani 189,475 sawa na fedha za kitanzania shilingi 30,316,000na mkia mmoja wa tembo na walipoendelea kufuatilia katika mizigo hiyo walibaini kuwepo kwa tiketi moja ya kusafiria  abiria ikiwa na namba zilizofutwafutwa na walipofuatilia kwenye kitabu cha tiketi waligundua kuwa tiketi hiyo ilikuwa imesajiliwa kwa jina moja tu
Na askari walipoendelea kufuatilia ilionekana abiria mwenye tiketi hiyo na mizigo hiyo iliyotiliwa mashaka aliamua kuitelekeza mizigo yake baada ya kuwaona askari polisi wakiwa kwenye upekuzi wa mabasi na hivyo mtu huyo hakuweza kufahamika na jitihada za polisi kwa kushirikiana na wananchi za kumtafuta zinaendelea ili aweze kufikishwa mahakamani .
Aidha kamanda Nsimeki ameendelea kuwaomba wananchi na raia wema kuendelea kutoa ushirikiano mwema kwa jeshi la polisi katika harakati za kuzuia biashara hiyo haramu inayoendelea kuhujumu uchumi wa taifa.
Katika tukio jingine lililotokea katika kijiji cha Langiro wilayani Mbinga mkoani Ruvuma  kamanda Nsimeki amesema tukio hilo lililotokea Julai 22 mwaka huu majira ya saa 7 usiku ambapo  mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Peter Kapinga(19) aliuawa baada ya kupigwa na mti kichwani na watuhumiwa wa tukio hilo ni Ingo Kapinga na Elias Kapinga ambapo chanzo niugomvi uliotokea kwenye disko na  ugomvi wao huo  ulisababisha kifo kwa sababu ya wivu wa kimapenzi ulioanzia kwenye muziki huo amba baada ya tukio hilo mtuhumiwa mmoja Inigo Kapinga alitoroka na mwenzake Elias Kapinga(14) alikamtwa na anahojiwa na polisikuhusina na tukio hilo.

Habari kwa hisani ya demashonews.blogspot.com

No comments:

Post a Comment