Picha ya pamoja
ZAIDI ya Tani 60,000 za Shayiri
zinatarajiwa kuvunwa kutoka kwa Wakulima wa Kanda ya Nyanda za Juu
Kusini baada ya kupatiwa mafunzo juu ya kilimo cha mazao yenye tija na uwepo wa
soko la uhakika.
Aidha zaidi ya Wakulima 400 kutoka Kanda hiyo
ndiyo walionufaika na Kilimo hicho na kujihakikishia Soko la zao ambalo
hutumika zaidi katika utengenezaji wa Vinywaji moto ambavyo ni Bia na
uzalishaji mwingine kutokana na uwepo wa Viwanda vikubwa vya kuzalisha vinywaji
hivyo.
Hayo yalibainishwa juzi na Meneja masoko wa
Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) Kanda ya Mbeya, Raymond Degera,wakati wa
Ziara ya Waandishi wa Habari katika Kiwanda cha Bia kilichopo Iyunga Jijini
Mbeya.
Alisema kutokana na uwepo wa Kiwanda cha
Bia Mkoani Mbeya na kuhudumia Wananchi wa Kanda ya Nyanda za Juu kusini waliona
si vema Malighafi zikatoka Nje ya Mikoa hiyo ili hali ardhi na hali ya Hewa
inaruhusu kilimo cha mazao hayo na kuamua kutoa elimu namna ya kunufaika na
Kilimo.
Degera alisema Kampuni ilianzisha Programu ya kuwawezesha
Wakulima kuhusu kilimo cha mazao yenye tija ambapo Wakulima wa Wilaya ya Mbozi,
Sumbawanga na Iringa wanaofikia 400 ambao waliitikia na kuanza uzalishaji ambao
baada ya mavuno kiwanda kitanunua moja kwa moja kutoka kwa wakulima ambao
wanatarajia kuvuna Tani 60,000.
Kwa upande wake Mpishi Mkuu wa Bia wa
Kampuni ya Tbl, Tito alisema Sheria za Tanzania zinatakiwa kusimamiwa ipasavyo
kuhusu matumizi ya Vilevi kwa kuwashtaki wanaozidisha pombe na wengine
wanaokunywa mida ya kazi na kuleta usumbufu kwa wengine.
Alisema Utaratibu wa Nchi zingine
huwalazimisha wananchi wake kutumia Chupa mbili za Bia kwa siku na kwamba
anayehitaji kuongeza zaidi ya hapo wauzaji huwakatalia, Sheria ambayo alishauri
kutumika ili kuongeza uzalishaji na kuiondoa nchi katika majanga yanayotokana
na ushawishi wa Pombe.
Aliongeza kuwa kama wamiliki na
watengenezaji wa Pombe wanahitaji wananchi wanywe kwa utaratibu ili waendelee
kuwa wateja wao na kusaidia kuchangia kodi kwa Taifa kutokana na Kampuni
hiyo kuongoza kwa kuchangia kodi katika pato la Taifa.
Aidha katika Ziara hiyo Wanahabari walipata
fursa ya kuelezwa sheria za unywaji wa Pombe na madhara yake, umri wa mtu
kuanza kunywa pombe pamoja na madhara yake ambapo baada ya zoezi hilo
walitembelea maeneo mbali mbali ya Kiwanda hicho.
Mbali na hilo wanahabari hao pia
walishindanishwa kuonja Bia na kuzitambua kwa majina zoezi ambalo lilikuwa gumu
kwa waandishi wengi huku Waandishi wanne wakiibuka washindi baada ya wawili
kushika nafasi ya kuanza kwa kupata alama tatu kati ya Tano ambao ni Emmanuel
Madafa na Joseph Mwaisango huku walioshika nafasi ya pili kwa kupata alama
mbili kwa tano wakiwa ni Joachim Nyambo na Kenneth Ngelesi.
Chanzo:Mbeyayetu.blogspot.com
|
No comments:
Post a Comment