Showing posts with label Swahlili news. Show all posts
Showing posts with label Swahlili news. Show all posts
Thursday, October 3, 2013
Mashine za TRA zazua balaa.. Mbeya wagoma kuzinunua, vurugu zazuka.....!
Mabomu ya machozi yalipigwa ili kuzuia wafanyabiashara wasilete vurugu
Wafanyabiashara hao walichoma matairi ili kuwazuia polisi wasiweze kuwafikia
Na Kenneth NgelesiWAFANYABIASHARA mkoani Mbeya wamezua kizaazaa wakigoma kufungua maduka wakipinga agizo la Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) linalowataka kununua mashine za kielektroniki kwa ajili ya kukatia risiti za wateja pindi wanapowauzia bidhaa.
Katika sokomoko hilo lililotokea jana na kusababisha taharuki kwa muda kadhaa, wafanyabiashara hao wanadai kuwa gharama za mashine zitolewe na serikali.(P.T)
Sunday, September 29, 2013
ukosefu wa elimu wasababisha UJINGA, MARADHI NA UMASKINI
Watoto wengi katika nchi zinazoendelea wanakabiliwa na tatizo la ujinga, maradhi na umaskini hivyo basi kupatikana kwa elimu bora kutawasaidia kujikwamua na matatizo hayo pindi watakapomaliza masomo yao na kupata ajira na hivyo kujikwamua na hali ngumu ya maisha. (HM)
Dk Shein ampongeza Rais wa China
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein amemtumia salamu za pongezi Rais wa China, Xi Jinping kwa kuadhimisha miaka 64 ya Uhuru wa nchi hiyo.
Wednesday, August 14, 2013
RAIS AFUNGUA MKUTANO MKUU
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,akifungua Mkutano wa mwaka wa Jumuiya ya Mahakimu na Majaji wa
Afrika Mashariki,(EAMJA) ulioanza leo katika Hoteli ya Zanzibar Beach
Resort nje ya Mji wa Unguja.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
M.M
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) pamoja na Majaji wa Nchi za Afrika Mashariki, wakisimama wakati wimbo wa Taifa wa Nchi hizo ukipigwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa mwaka kwa Nchi hizo,ambao utakchukua siku tatu katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel,iliyopo nje ya Mji wa Unguja.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.
Tuesday, August 6, 2013
Baraza la jiji lamuomba radhi Mandela
Maafisa wakuu mjini Johannesburg, wamemuomba radhi Nelson Mandela kwa kumtumia kimakosa hati ya kudai malipo pamoja na onyo kuwa huenda akakatiwa huduma ya maji na stima kwa kuchelewa kulipia huduma hizo. (HM)
Walisema kuwa onyo hilo linalomtaka Mandela alipe dola 660 la sivyo akatiwe huduma hizo ilipaswa kutumwa kwa mtu mwingine wala sio Mandela.
Maafisa wa baraza la jiji wamekuwa wakipokea malalamiko mengi kutoka kwa wakaazi kuhusu hati za madai ya malipo ya huduma wanazopokea kutoka kwa baraza la jiji.
Mandela amekuwa hospitalini tangu tarehe 8 mwezi Juni akitibiwa homa ya mapafu.
"baraza la jiji lingependa kuomba radhi familia ya Mandela kwa kwa athari zozote zilizotokana na jambo hili,''
Notisi ya baraza la jiji ilitishia kukomesha huduma hizo na hata kuchukua hatua za kisheria ikiwa deni hilo la siku 30 halingelipwa.
Hata hivyo, msemaji wa baraza hilo Kgamanyane Maphologela alielezea kuwa anwani na nambari ya akaunti ya kulipia zilikuwa za mteja mwingine ambaye ni jirani wa Mandela.
Vile vile nambari ya barabara na jina la mteja zilikuwa sawa , ila mteja anaishi katika sehemu tofauti.
Bwana Maphologela alisema kuwa hatua zitachukuliwa dhidi ya wale waliofanya kosa hilo.
Familia ya Mandela, ambayo makaazi yake yako katika mtaa wa kifahari wa Houghton, daima hutembelewa na watu wenye nia ya kuiafriji familia ya Mandela, kumtakia afya njema rais huyo wa zamani.
Mwezi jana makao makuu ya chama cha kitaifa cha ANC, inasemekana kilipokea kimakosa hati za kudaiwa randi milioni 3.5.
Mandela ambaye ni rais wa kwanza wa Afrika Kusini kuchaguliwa kidemokrasia, anatazamiwa na wengi kama baba wa taifa.
Aidha Mandela alifungwa jela kwa miaka 27 baada ya kuanzisha harakati dhidi ya uliokuwa utawala wa kibaguzi. Chanzo: bbcswahili
Monday, August 5, 2013
Mgombea alitumia Ziwa Nyasa kujipigia debe Malawi
Mutharika, ambaye ni mwanasheria, aliyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika juzi Mkoa wa Kati.
Akikaririwa na gazeti la Nyasa Times, Mutharika alisema Tanzania haina cha kuambulia kwa Ziwa Malawi.
Kiongozi huyo ambaye hakuwapo katika mkutano wa Rais Joyce Banda na wapinzani kuzungumzia mustakabali wa ziwa, aliwahakikishia Wamalawi kuwa wasiwe na wasiwasi wa mvutano huo.
Mutharika ziwa lote ni mali ya Malawi na akisisitiza kuwa, Tanzania haina hata punje ya eneo.
“Hakuhitajiki majadiliano, Ziwa Malawi ni mali ya Malawi, litakuwa la Malawi,” alisema Mutharika ambaye alichukua masomo ya Sheria Tanzania.
“Tanzania inatumia nafasi ya udhaifu wa uongozi wetu, lakini ukweli, hawana hata tone la eneo... Tutakapoitwa kwenye uchaguzi ujao mwakani, tutamaliza haya yote. Nitaleta meli nyingi kwa ajili ya maendeleo ya uchumi, kutengeneza ajira za kutosha kwa vijana,” alisema Mutharika huku akishangiliwa na wafuasi wake.
Tanzania inataka kugawana ziwa, lakini Malawi imegomea mpango huo na suala hilo liko katika majadiliano ambayo Banda alisema kama mwafaka haukupatikana ifikapo Septemba 30, Malawi itapeleka suala hilo Mahakama ya Kimataifa (ICJ).
Chanzo: mjengwa blog.

Subscribe to:
Posts (Atom)