Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein amemtumia salamu za pongezi Rais wa China, Xi Jinping kwa kuadhimisha miaka 64 ya Uhuru wa nchi hiyo.
Katika salamu zake hizo, Rais wa Zanzibar amesema wananchi wa Zanzibar wanaungana na ndugu zao wa China katika kusherehekea miaka 64 ya uhuru wa nchi hiyo pamoja na urafiki na mshikamano uliodumu kwa muda mrefu baina ya mataifa hayo mawili.(P.T)
Dk Shein ameitumia fursa hiyo
kuipongeza Serikali ya China kwa mafanikio makubwa iliyoyapata katika
sekta zote za maendeleo chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti.
Ameelezea matumaini yake kuwa ushirikiano baina ya Serikali ya China na Wananchi wa Zanzibar utaendelea kuimarika zaidi.
Ameelezea matumaini yake kuwa ushirikiano baina ya Serikali ya China na Wananchi wa Zanzibar utaendelea kuimarika zaidi.
No comments:
Post a Comment