Katika dunia ya leo, wengi wetu tumekuwa tukifanya kazi kwa muda mwingi, hata kutufanya tukose muda wa kufanya mazoezi. Siku hizi, wengi wa wafanyakazi wamekuwa kwenye magari, ofisini kwenye kiti kurudi tena kwenye gari na kulala, hivyo hukosa hata muda wa kupasha / kunyoosha viungo.
Katika dondoo ya leo, tutakufahamisha moja ya mazoezi yenye matokeo mazuri kwa viungo vya binadamu tena bila ya kutumia kifaa chochote. Na hii si nyingine bali ni Push up. Push up ni moja ya mazoezi yanayojenga afya njema kwani push up zinasaidia kuimarisha kifua, mabega misuli ya mikono.
Jinsi ya kufanya push up: Uso wako ukiwa unatizama chini, weka mikono yako kwenye sakafu, itanue izidi kidogo mabega yako (kama inavyoonekana kwenye picha). Hakikisha vidole vyako vya miguu vipo sakafuni, kama hii ni ngumu, basi unaweza kuanza kwa kuweka magoti yako chini. Hakikisha mwili wako umenyooka kuanzia vidoleni hani kichwani. Kunja mabega yako mpaka uwe kama unagusa sakafu. Rudi juu kwa kujinyanyua kwa kutumia mabega, hakikisha mwili wako umenyooka mwanzo hadi mwisho. Fanya hivi mara kadhaa ukiwa unaongeza idadi siku hadi siku.
Hauna haja ya Gym, hauna haja ya kununua kifa chochote, unaweza kufanya zoezi hili hata ukiwa ofisini. Na hii ndio dondoo ya leo.
No comments:
Post a Comment